QR Code: oW31HyXT0L

Ripoti hii inawasilisha matokeo, mapendekezo na hitimisho kutoka katika kaguzi za taarifa za fedha na uzingatiaji wa sheria kwa wakala na taasisi mbalimbali za serikali. Kaguzi hizi zilihusisha taasisi mbalimbali zikiwemo mafungu (votes) ya wizara 64 na idara za Serikali, balozi 43, wakala wa serikali 30, mifuko maalum ya fedha 19, vyama vya siasa 19, hospitali za rufaa na maalumu 34, Taasisi nyingine 129 na kaguzi maalum tatu. Aidha, kaguzi hizi zilihusisha mamlaka ya mapato Tanzania, Hesabu za mfuko mkuu, na ukaguzi wa majalada ya Pensheni kwa mwaka wa fedha unaoishia tarehe 30 Juni 2022.