Ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2018-2019 ni pamoja na Ripoti ya Ukaguzi wa Serikali kuu, Ripoti ya Ukaguzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, Ripoti ya Ukaguzi wa Mashirika ya Umma, Ripoti ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo, Ripoti ya Ukaguzi wa Mifumo ya TEHAMA na Ripoti ya Ukaguzi wa Ufanisi.