“Mamlaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali yameainishwa chini ya Ibara ya 143 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuainishwa katika Vifungu vya 10, 11 na 12 Vya Sheria ya Ukaguzi wa Umma.”
“Kukagua mapato na matumizi ya serikali kama ilivyoidhinishwa na Bunge ili kuleta uwajibikaji na uwazi zaidi katika usimamizi wa rasilimali za umma.”
“Sheria zimempa mamlaka CAG ya kuchunguza na kukagua hesabu za maofisa masuuli na wakusanyaji mapato kwa niaba ya Bunge.”